Monday, 20 July 2015

KAGASHEKI ARUDISHA FOMU ZA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BUKOBA MJINI.KAGASHEKI ARUDISHA FOMU ZA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BUKOBA MJINI.e Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Sued Kagasheki anaemaliza muda wake

August 20 mwaka huu, leo amerudisha fomu za kugombea ubunge katika jimbo la Bukoba mjini kupitia ccm,akiongea na wanachama waliomsindikiza amewahakikishia kuwa wasiwe na wasiwasi jimbo litabaki mikononi mwa ccm,amewakumbusha kipindi cha nyuma wakati jimbo lilipo kuwa mikononi mwa upinzani adha kubwa walizokutano nazo,lakini pia amesema katika kipindi cha ubunge wake yapo mambo mengi sana yamefanyika, japo wapo watu wanatumia kila njia kusambaza propoganda za kupotosha, lakini akasema uwezi kuzuia mtu kusema kile anachokiamini,akasema kuna watu katika dunia hii hawaamini kama mungu yupo,sasa mimi Kagasheki ni nani nipendwe na wote? kuna watu walimkataa yesu na wengine mtume,lakini si kitu hao waache, waliowengi wanatambua kazi tulizofanya na tutazieleza wakati ukifika.Wengine waliorudisha fomu ni Bw George PhilbR ubaiyuka, Eliet Projestus, Philbert Katabazi,Anatory Aman na Mujuni Kataraiya aliepoteza jimbo mwaka 2000 na kuchukuriwa na Wilfred Rwakatare na kuchukuliwa na Balozi Kagasheki 2005 na 2010.
Wanachama wakimpungia Balozi Kagasheki.Balozi Kagasheki akiongea na wanachama.

Wanaccm waliojitokeza kumsindikiza Balozi Kagasheki kurudisha fomu.


Mwenyekiti wa kata ya Bilele Taofiq sharifu akitoa msimamo wa bilele.

Katibu wa kata ya hamugembe bw Hamza akieleze msimamo wa kata ya Hamugembe.
Balozi Kagasheki akisaini kitabu cha uthibitisho wa kurudisha fomu.


Balozi Kagasheki akizungumza na wanachama wa ccm na wapenzi waliomsindikiza kurudisha fomu.

No comments:

Post a Comment